Saturday, September 13, 2014


MENEJA wa Swansea City Garry Monk ameshinda Tuzo ya Wadhamini Barclays ya Ligi Kuu England na kutajwa ndie Meneja Bora wa Mwezi baada ya kuongoza Timu yake kushinda Mechi zote Tatu za Ligi Kuu England.
Swansea wamefungana kileleni na Chelsea ambao wako juu kwa ubora wa Magoli na Meneja wao Jose Mourinho alikuwemo kwenye kugombea Umeneja Bora wa Agosti.


Diego Costa akiwa amebeba tuzo yake ya Mwezi Agosti
Kwa upande wa Wachezaji Straika wa Chelsea Diego Costa, ambae ameifungia Timu yake Bao katika kila Mechi ya Ligi waliyocheza, ndie amechaguliwa Mchezaji Bora na kumbwaga mwenzake wa Chelsea Cesc Fabregas na Nathan Dyer pamoja na Gylfi Sigurdsson wa Swansea, na Andreas Weimann wa Aston Villa.

Jumamosi Swansea na Chelsea zitakutana USO KWA USO huko Stamford Bridge.

WACHEZAJI WALIOKUWA WANAGOMBEA NAFASI HIYO:
Diego Costa (Chelsea)
Cesc Fabregas (Chelsea)
Nathan Dyer (Swansea)
Gylfi Sigurdsson (Swansea)
Andreas Weimann (Aston Villa)

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog