Saturday, September 13, 2014



Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akimkabidhi Ngao ya Jamii nahodha wa timu ya KMKM, Khasim Ali baada ya kuifunga Shaba ya Pemba 2-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar juzi. Kulia ni Meneja Mauzo wa kinywaji cha Grandmalt, Kassiro Msangi. (Na Mpiga Picha Wetu)
Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na mmoja wa wachezaji wa timu ya soka ya KMKM wakati akikagua timu hizo kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii baina ya KMKM na Shaba ya Pemba kabla ya ufunguzi wa ligi kuu ya soka ya Grandmalt inayotarajiwa kuanza jumatatu tarehe 15/09/2014, KMKM ilishinda kwa mabao 2:0 dhidi ya shaba ya Pemba.

Sehemu ya washabiki waliofurika kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar kushudia mchezo kati ya KMKM na Shaba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog