Saturday, September 13, 2014



Daley Blind signs for Manchester United
Louis van Gaal anaamini kumaliza kwenye Tatu Bora katika Ligi Kuu England Msimu huu ni lengo ambalo linaweza kufikiwa.
Msimu uliopita, chini ya Meneja alietimulia David Moyes, Man United walimaliza Nafasi ya 7 na kukosa kucheza Mashindano ya UEFA Ulaya.Juzi, akiongea na Wawekezaji na pia kutangaza Mapato ya Rekodi, Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Man United, Ed Woodward, alisema Bajeti zao zijazo zimeweka na kukadiriwa kwa Misingi ya kumaliza katika Nafasi 3 za juu.

Jana Meneja wa Man United, Louis van Gaal, ameunga mkono lengo hilo na kusema: “Sidhani kama ni lengo ambalo haliwezekani. Klabu kama Manchester United ni lazima iweke malengo. Hata mie naweka malengo. Kuwemo 3 bora ni sahihi kwa sababu Manchester United inataka kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI!”

Wakiwa na Pointi 2 tu na Goli 2 katika Mechi zao 3 za kwanza za Ligi, Man United inabidi washinde Mechi yao ya Jumapili dhidi ya QPR Uwanjani Old Trafford na Mechi hii huenda ikiwaona Wachezaji wao wapya Radamel Falcao, Marcos Rojo, Daley Blind na Luke Shaw, wakicheza kwa mara ya kwanza huku mpya mwingine, Angel Di Maria, akicheza kwa mara ya kwanza Uwanjani Old Trafford.

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumamosi Septemba 13

14:45 Arsenal v Man City
17:00 Chelsea v Swansea
17:00 Crystal Palace v Burnley
17:00 Southampton v Newcastle
17:00 Stoke v Leicester
17:00 Sunderland v Tottenham
17:00 West Brom v Everton
19:30 Liverpool v Aston Villa

Jumapili Septemba 14
18:00 Man United v QPR
Jumatatu Septemba 15
22:00 Hull v West Ham

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog