ARSENE Wenger kesho anawakabili mabingwa watetezi wa ligi kuu soka nchini England, Manchester City katika mchezo wa ligi kuu uwanja wa Emirates.
Baada ya kumsajili Danny Welbeck, je, kikosi kitakakuwa kama inavyoonekana pichani juu?
Kuna majeruhi wachache waliojitokeza kwenye mechi za kimataifa ambao ni Aaron Ramsey, Mikel Arteta na Mesut Ozil.
Lakini inaonekana Wenger ana chaguo kubwa la wachezaji na wataweza kumsaidia katika mechi ya kesho.
Danny Welbeck akiwa katiika mazoezi ya Arsenal uwanja wa London Colney leo
Arsene Wenger ana wachezaji wengi wanaoweza kumsaidia kwenye mechi dhidi ya Manchester City kesho jumamosi.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumamosi Septemba 13
14:45 Arsenal v Man City
17:00 Chelsea v Swansea
17:00 Crystal Palace v Burnley
17:00 Southampton v Newcastle
17:00 Stoke v Leicester
17:00 Sunderland v Tottenham
17:00 West Brom v Everton
19:30 Liverpool v Aston Villa
Jumapili Septemba 14
18:00 Man United v QPR
Jumatatu Septemba 15
22:00 Hull v West Ham
0 maoni:
Post a Comment