Saturday, September 13, 2014


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kesho Jumamosi (Septemba 13 mwaka huu) saa 4 asubuhi litaendesha mafunzo ya matumizi ya tiketi za elektroniki kwa wadau wa mpira wa miguu Dar es Salaam.
Mafunzo hayo Uwanja wa Taifa, na kushirikisha wasimamizi wa mechi, viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na makatibu na maofisa habari wa klabu za Azam na Yanga.
Washiriki wengine wa mafunzo hayo ni Meneja wa Uwanja wa Taifa na msaidizi wake, wasimamizi wa milangoni (stewards), waandishi wa habari wa Dar es Salaam maofisa usalama wa TFF.
Mafunzo hayo yatahitimishwa Jumapili (Septemba 14 mwaka huu) kwa mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Azam na Yanga kuanzia saa 10 kamili jioni.
Tiketi zimeanza kuuzwa jana (Alhamisi) kupitia M-Pesa, CRDB Simbanking na maduka ya Fahari Huduma.

BONIFACE WAMBURA
MKURUGENZI WA MASHINDANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

MAKOCHA YANGA, AZAM FC LEO KUKUTANA NA WANAHABARI
Makocha wa Timu za Azam FC na Young Africans SC watakutana na Waandishi wa Habari hii Leo.
Mkutano huo utafanyika Leo Jumamosi (Septemba 13 mwaka huu) Saa 5 Asubuhi katika Ofisi za TFF zilizopo ghorofa ya tatu kwenye Jengo la PPF Tower.
Makocha hao watazungumzia jinsi walivyoandaa vikosi vya kwa ajili ya mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) itakayochezwa Jumapili (Septemba 14 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog