LOUIS van Gaal amesema Danny Welbeck aliuzwa Arsenal kwasababu hakuwa mzuri sana kwa Manchester United, lakini amekataa kuwa klabu imeharibu sera yake ya soka la vijana.
Majira ya kiangazi, United walitumia paundi milioni 150 katika usajili wa wachezaji wapya, wakiwemo Angel di Maria na Radamel Falcao.
Kitendo hicho kimezua maswali kuwa klabu hiyo imewageuzia mgongo wachezaji vijana waliokulia katika akademi yao, hususani baada ya kumuuza mshambuliaji wa England, Welbeck kwenda klabu ya Arsenal kwa dau la paundi milioni 16.
Lakini katika mkutano na waandishi wa habari wa kuwatambulisha Falcao na Daley Blind jana alhamisi, Van Gaal alidai kuwa United bado itajikita kuwakuza wachezaji vijana.
Wachezaji wapya waliosajiliwa na Arsenal (kutoka kushoto) Mathieu Debuchy, Calum Chambers, David Ospina, Danny Welbeck na Alexis Sanchez katika uwanja wa mazoezi wa London Colney jana alhamisi.
Van Gaal alieleza sababu za kumuuza Mzaliwa wa Manchester, Welbeck ambaye ameichezea klabu hiyo toka utotoni, akisema kuwa rekodi ya mshambuliaji huyo ya mabao 29 katika mechi 142 haikaribiani na ya Wayne Rooney au Robin van Persie.
"Niliwapa wachezaji wote nafasi ya kunishawishi," alisema Van Gaal. "Unapouliza kuhusu Welbeck, alikuwepo hapa tangu akiwa na miaka 9 na baada ya kwenda kwa mkopo Sunderland, alicheza misimu mitatu United, lakini hajawa na rekodi kama ya Van Persie au Rooney. Ndio maana tulimuacha aende".
0 maoni:
Post a Comment