Je ushawahi kushabikia smechi ya kandanda baina ya mahasimu wawili wa jadi ?
Sasa hebu fikiria Mashabiki wa mechi ya fainali kuwa ni Viongozi wa kidini .
Taswira hiyo huenda ikakamilika
siku ya jumapili Papa Francis ambaye ni Raiya wa Argentina akitizama
mechi baina ya Argentina na Ujerumani na Papa mtangulizi wake Benedicto
16 raiya wa Ujerumani.
Makao makuu ya Kanisa Katoliki hata hivyo
imekuwa wazi ikisema kuwa hilo huenda lisikamilike kwani papa Benedicto
sio shabiki sugu ukimlinganisha na papa Francis ambaye ni shabiki sugu
wa Argentina.
Msemaji wa Vatican Federico Lombardi akisema
kuwa labda kadinali mkuu wa zamani wa Buenos Aires Jorge Bergoglio
yaani papa Franci atatizama fainali hiyo.
Papa Benedict XVI, 87, anajulikana kuwa msomi na
pia mwenye uraidbu wa mziki wa ala mara nyingi akipapasa roho yake kwa
kucheza piano .
Wangdani wa Vatican ahata hivyo wanasema kua
katika enzi zake Papa Benedict XVI alikuwa hawezi kosa matokeo ya mechi
za klabu anayoishabikia ya Bayern Munich.
Gazeti moja la Italia''the Osservatore Romano''
ndilo lililotibua uvumi huu lilipochapisha habari kabla ya kuanza kwa
kombe la dunia lilipobashiri kuwa Argentina itakutana na Ujerumani
katika fainali ya kombe la dunia na hivyo kushuhudia mashabiki wa haiba
yake , papa Benedicto wa 16 na papa Francis .
0 maoni:
Post a Comment