Kwenye rada: Beki wa Atletico Madrid, Javi Manquillo anatakiwa na Arsenal.
KLABU ya Arsenal inafanya jitihada za kumsajili beki wa kulia wa Atletico Madrid , Javi Manquillo.
Washika
mtutu hao wa London wanataka kumsajili beki huyo wa Hispania kwa lengo
la kuongeza ushindani katika nafasi ya beki wa kulia msimu ujao.
Kama
watakamilisha usajili huo, basi Manquillo atachuana katika nafasi hiyo
na beki waliomsaini siku chache zilizopita, Mathieu Debuchy.
Njiani kusepa: Carl Jenkinson anaweza kuondoka Asernal na anawindwa zaidi na Newcastle.
0 maoni:
Post a Comment