Tabasamu
kubwa: Mshambuliaji wa Man City ambaye hajatulia , Alvaro Negredo
akicheka wakati alipokuwa anapenda ndege kwenda Dundee.
KIKOSI
cha mabingwa wa England, Manchester City kimekwea pipa kwenda Dundee
tayari kuanza ziara yao ya maandalizi ya msimu huko Scottish.
Katika
msafara huo, pia umemjumuisha mshamabiliaji ambaye hajatulia kwa sasa,
Alvaro Negredo aliyeonekana kuwa katika morali nzuri.
Kikosi
cha Manuel Pellegrini kitacheza Dundee siku ya jumapili kabla ya
kusafiri siku inayofuata kwenda Edinburgh kucheza dhidi ya Hearts siku
ya ijumaa.
Negredo
anayehusishwa kuondoka Etihad, alipigwa picha akipanda ndege binafsi ya
Man City, `City Jet` jana jioni, huku naye kipa mpya, Willy Caballero
akiwemo katika msafara huo.
0 maoni:
Post a Comment