Gwiji: Mourinho (kushoto alimleta Drogba katika klabu ya Chelsea mwaka 2004 akitokea Marseille ya Ufaransa.
KLABU ya Chelsea inaangalia uwezekano wa kumrudisha Didier Drogba katika dimba la Stamford Bridge.
Nyota huyo mwenye miaka 36
anazivutia klabu za Qatar, wakati Juventus nao wakifikiria kumnasa
mkongwe huyo anayecheza katika klabu ya Galatasaray ya Uturuki.
Bado Jose Mourinho ana mahusiano mazuri na Muivory coast huyo na anavutiwa kumrudisha kwa majukumu ya ukocha zaidi.
Mkongwe huyu wa miaka 36 anazivutia klabu za Qatar, nao Juventus wanaitaka saini yake.
Klabu
hizo za Qatar zinatarajia kutoa ofa nono na mshahara utajadiliwa,
lakini unakadiriwa kuwa paundi milioni 3 kwa msimu baada ya makato ya
kodi.
Wazo la kurudi Chelsea litaangaliwa zaidi na pande zote.
0 maoni:
Post a Comment