Hisia:
Neymar alimwaga machozi, huku akiweka wazi kuwa alikaribia kuwa kichaa
baada ya Juan Zuniga kumfanyia faulo mbaya kwenye mchezo wa robo fainali
ya kombe la dunia dhidi ya Colombia.
NYOTA wa Brazil, Neymar Jr
amefichua siri kuwa alishindwa kuzuia machozi na alikaribia kuwa kichaa
baada ya kugongwa na Juan Zuniga na kuvunjika mfupa wa uti wa mgongo.
Neymar kwa mara ya kwanza
alifanya mkutano na waandishi wa habari baada ya kutoka Hospitalini
ambapo anauguza majeraha yake ya mfupa wa uti wa mgongo uliovunjika
kwenye mechi ya robo fainali ya kombe la dunia dhidi ya Colombia.
Machozi: Neymar alishindwa kuendelea kucheza fainali za kombe la dunia baada ya kuvunjika mfupa wa uti wa mgongo.
Pia
Neymar hajakubaliana na maneno ya wakala wake aliyemuita Luiz Felipe
Scolari kuwa ni kocha mbaya, mwenye majivuno na aliyepitwa na wakati.
0 maoni:
Post a Comment