Shirikisho la soka Duniani FIFA
limekatalia mbali ombi la rufaa la mchezaji wa Uruguay Luis Suarez
dhidi ya marufuku yake ya mizi minne kwa kosa la kumng'ata Mlinzi wa
Italia .
Katika barua kwa wanahabari FIFA ilisema kuwa
imekatialia mbali ombi la Shirikisho la Soka la Uruguay la kuitaka
kupunguza adhabu ya Mshambulizi huyo wa Liverpool .
Hata hivyo
Suarez anauhuru wa kukata rufaa katika mahakama ya rufaa ya michezo
(Court of Arbitration for Sport) iwapo hataridhika na Uamuzi huo.
Mshambulizi huyo wa Liverpool alibanduliwa nje ya kombe la dunia baada
ya tukio hilo la Juni tarehe 24 na sasa anaomba msamaha ili iwe rahisi
kwake angalau kujifua pamoja na wachezaji wenza huko Anfield Uingereza
huku akitarajia uhamisho kuelekea Uhispania katika klabu ya Barcelona .
0 maoni:
Post a Comment