Carlos
Queiroz alijiuzulu nafasi yake ya ukocha wa timu ya taifa ya Iran baada
ya nchi hiyo kutolewa hatua ya makundi katika fainali za kombe la dunia
mwaka huu nchini Brazil.
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Mtandao
0712461976
HAPA tunaangalia kwanini Asia imeshindwa kufanya vizuri katika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
1. UKOSEFU WA UONGOZI
Wakati kocha wa Korea Hong Myung-bo
anasafiri kwenda Uholanzi mwezi machi mwaka huu kumtembelea Park
Ji-sung, hakwenda kuangalia wachezaji muhimu bali ni kumshawishi nyota
huyo aachane na mpango wa kustaafu soka la kimataifa.
“Timu ya vijana inahitaji
wakongwe,” alisema Hong. Park alipotezea wazo lile, lakini ni ukweli
kuwa Korea ilikosa wachezaji wenye uzoefu na viongozi kama yeye. Pia
Japan haikuwa na wachezaji ambao wangepewa majukumu ya kuwaongoza vijana
uwanjani katika mazingira tofauti tofauti ya mechi.
2. MAKOSA YA MAKOCHA
Alberto Zaccheroni alikuwa na
maandalizi kamili yaliyochukua hadi miaka minne tangu alipokabidhiwa
timu ya Japan, lakini bado kocha huyo raia wa Italia hajaweza kuonesha
kiwango kizuri katika hatua ya makundi. Japan ilicheza mpira wa kawaida
dhidi ya Ivory Coast na Ugiriki.
Alikosolewa kwa kumuanzisha
Yasuhito Endo dhidi ya Waafrika, pia aliendelea kumuacha Yasuyuki Konno
katika idara ya ulinzi wakati alishindwa kufanya kazi yake na
angemtumia hata Zaccheroni kutokana na kiwango chake kuwa kizuri kwa
wakati ule.
Kocha
wa Korea, Hongg, hakuwa na wachezaji wenye uzoefu, lakini alishindwa
kuwatumia vijana wake katika safu ya ulinzi na hakusikiliza ushauri wa
vyombo vya habari na mashabiki na kuendelea kumtumia mshambuliaji butu
Park Chu-young. Carlos Queiroz alikuwa na kiwango kizuri, labda atajuta
baada ya kushindwa kuonesha ubora wake na kuisaidia timu kwenye mechi
dhidi ya Bosnia.
0 maoni:
Post a Comment