Wednesday, February 19, 2014


Well jel? Gareth Bale (R) looks on as youngster Jese receives praise for another goalscoring performance
Winga anayechipukia wa Real Madrid, Jese Rodriguez ameweza kuziba pengo la Cristiano Ronaldo vyema kipindi hiki ambacho anatumikia adhabu ya kadi nyekundu. Kukosekana kwa Ronaldo kulitafsiriwa na wengi kuwa itakuwa ni nafasi nzuri kwa Gareth Bale kuonekana, lakini Jesse ameweza kumfunika vibaya Bale kiasi ambacho kimemfanya macho ya mashabiki kuhamia kwa Jesse. Kutambua kiwango cha Jesse, kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti pia ameanza kumpa kipaumbele mchezaji huyu kwa kumpa namba kwenye kila mchezo. Jesse anaonekana kuwa ni mchezaji atakayeweza kusaidiana na Ronaldo kuibeba timu na hakika nafasi yake kwenye kikosi cha timu ya taifa la Hispania itaonekana kwa kuanza kucheza kwenye kikosi cha kwanza, kwani hadi sasa bado haiwahi kucheza kwenye timu ya kwanza ya taifa. 

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog