Wednesday, February 19, 2014

Messi akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza kwa penalti usiku huu Uwanja wa Etihad
BARCELONA imejiwekea mazingira mazuri ya kupenya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Manchester City, Uwanja wa Etihad usiku huu katika mchezo wa kwanza, hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo.

Lionel Messi alifunga bao la kwanza dakika ya 54 kwa penalti ya utata, baada ya yeye mwenyewe kuangushwa nje kidogo ya eneo la hatari na Martin Demichelis, lakini refa akatenga tuta, kabla ya beki Dani Alves kufunga la pili dakika ya 90. 

Hilo linakuwa bao la kwanza kabisa Messi anafunga dhidi ya vigogo wa Ligi Kuu ya England tangu ameanza kukutana navyo akiwa na Barca mwaka 2006 na kumaliza ukame wa kucheza saa 12 nchini humo bila kufunga.
Katika mchezo mwingine wa leo 16 Bora Ligi ya Mabingwa, Uwanja wa BayArena mjini Leverkusen, wenyeji Bayer 04 Leverkusen walichapwa mabao 4-0 na Paris Saint-Germain FC ya Ufaransa.
Mabao ya PSG yalifungwa Matuidi dakika ya tatu, pasi ya Verratti, Ibrahimovic dakika ya na 42 pasi ya Matuidi na Cabaye dakika ya 88 pasi ya Lucas.
 
 Wenyeji Manchester City wakicheza na  Barcelona katika Uwanja wa Etihad kipindi cha kwanza kilimalizika wakiwa bado 0-0 hakuna aliyeziona nyavu za mwenzake...
Kipindi cha pili dakika ya 54 Messi anaipatia bao timu yake Barcelona kwa mkwaju wa penati baada ya kukwatuliwa chini eneo hatari ndani ya box na mwamuzi J. Eriksson akamtoa kwa kadi nyekundu  mchezaji wa City Martín Demichelis aliyefanya mafyongo kwa kumtega Messi.  Dakika za majeruhi dakika ya 90 Dani Alves akawaongezea bao jingine Barcelona kwa kufanya 2-0 dhidi ya City baada ya kupewa pasi safi na Neymar.

Mchezaji wa Manchester City Aleksandar Kolarov akichuana na Dani Alves wa Barcelona
Kipa wa Barca Victor Valdes akionesha kiwango kwenye lango lake na kutowapa upenyo City kufunga!
 Martin D
Marching orders: Demichelis is shown a red card by referee Jonas ErikssonREDNje!!! 

 




































0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog