Monday, November 17, 2014


Kipa wa Manchester United David De Gea amezidi kuleta kizaazaa Klabuni kwake baada ya kujiunga na Listi ndefu ya Majeruhi alipoteguka Kidole kidogo cha Mkononi akiwa Mazoezini na Spain.

Shirikisho la Soka la Spain, RFEF, limethibitisha kuumia kwa De Gea, mwenye Miaka 24, na kusema ataikosa Mechi ya Leo hii YA Kundi C la EURO 2016 kati ya Spain na Belarus itakayochezwa huko Huelva Nchini Spain.

Hata hivyo, De Gea bado yupo chini ya uchunguzi wa Jopo la Madktari wa Spain ambao watatoa uamuzi kama Kipa huyo arudishwe Klabuni kwake Man United au la.

Majuzi, Kiungo wa Man United, Michael Carrick, nae alipata maumivu ya Nyonga akiwa na Timu ya Taifa ya England na kuondoka Kambini kurudi Manchester.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog