Monday, November 17, 2014



MWANAMICHEZO ambaye anacheza kwa kutumia pikipiki Bian Capper kutoka nchini Afrika kusini ametoa wito kwa watanzania kucheza mchezo huo ambao mbali ya kufurahisha pia unatumia akili na kukufanya uwe mkakamavu wakati wote.

Akizungumza jana kabla kuonesha umahiri huo mchezaji wa pikipiki ambaye ni raia wa Afrika Kusini anayefanya ziara katika nchi za Afrika kwa udhamini wa kinywaji cha Redbull atakuwa nchini kwa ziara za ya maonesho ya kuonesha namna ya kucheza na pikipiki kwa siku tatu.


Onyesho la kwanza lilianza jana kwenye viwanja vya Coco beach , leo Jumapili atakuwa Mlimani City na kesho Jumatatu atakuwa katika eneo la Ubungo Tanesco ambako litakuwa onyesho lake la mwisho.

Capper amesema kwamba amefurahia kuweza kufika nchini pia tayari ameshafanya maonyesho yake katika nchi za Kenya na Uganda.



Wakati huohuo Rais wa Tanzania Motorcross Acrobatic Club Blagina Mwihava alisema kwamba wamemleta mwanamuchezo huyo ambaye wana imani kubwa ataleta msisimko mkubwa kwa vijana wa kitanzania kuweza kupata hamasa ya kucheza mchezo huo wenye mvuto. 

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog