Monday, November 17, 2014



www.bukobasports.com
Hatimaye ile Filamu iliyokuwa ikisubiriwa sana na Wadau pamoja na Wapenzi wa Filamu Nchini ambayo Imechezwa na Wasanii kutoka Nchini Tanzania wakiwemo Slim Omary, Hashim Kambi, Irene Paul na Staa wa Filamu Kutoka Nchini Ghana Van Vicker iitwayo NEVER GIVE UP iliyochezwa Nchini Tanzania tayari imeshaingia Sokoni na Sasa inapatika katika Maduka yote ya Kuuza Filamu hapa Nchini. Vilevile ni filamu ambayo inatarajiwa kufanya vizuri sana katika Soko la Filamu Nchini na Nje ya Nchi.

Filamu ya NEVER GIVE UP ni filamu nyingine kutoka Kampuni ya Proin Promotions ambayo imeingia Sokoni Huku ikiwa imetanguliwa na Filamu mpya ya Lulu iitwayo MAPENZI YA MUNGU ambayo ipo sokoni wiki ya tatu sasa huku ikiendelea kufanya vizuri sana. Kabla hata ya FIlamu ya NEVER GIVE UP kuingia Sokoni tayari Kampuni ya Proin Promotions Ltd ilishapokea oda ya Nakala zisipongua Elfu 30 kutoka sehemu mbalimbali ndani ya Nchi ya Nje Ya Nchi.

Na Kama wewe pia unahitaji Filamu hii kwa bei ya Jumla unaweza kupiga Simu 0712 390 200 na Kufanya Oda yako

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog