TIMU
ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys
imelazimishwa suluhu pacha ya bila kufungana dhidi ya Afrika Kusini,
(Amajimbo) katika mchezo wa kwanza wa raundi ya pili kuwania tiketi ya
kucheza Fainali za Afrika za vijana.
Mchezo huo ulipigwa katika dimba la kisasa la Azam Complex, Chamazi, , Mbande, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, dakika 20 za
kwanza, Afrika kusini walitawala na kulisumbua lango la Serengeti Boys,
lakini mchezo huo ukabadilika na vijana wa Tanzania kuanza kusakata soka
la uhakika.
Katika kipindi hicho cha kwanza,
Serengeti walipata nafasi mbili za wazi, lakini washambuliaji wake
walishindwa kuzibadili kuwa magoli.
0 maoni:
Post a Comment