Mashambulizi yameanza: Mourinho ameanza kuishambulia Asernal kwa maneno ikiwa umebaki mwezi mmoja kuanza kwa msimu mpya.
Imechapishwa Julai 19, 2014, saa 1:45 asubuhi
KOCHA wa Chelsea , Jose Mourinho
ameipiga madongo mawili Asernal zikiwa zimesalia siku 29 tu kuanza kwa
mitanange ya ligi kuu soka nchini England.
Mreno huyo akizungumza kama balozi wa
BT Sport alidai kiungo aliyemsajili, Cesc Fabregas kamwe hakutaka kurudi
Emirates majira ya kiangazi mwaka huu na alisema Jack Wilshere
ameonesha mfano mbaya kwa watoto baada ya kukutwa akivuta sigara kwenye
Las Vegas wiki iliyopita.
Mourinho alifanikiwa kumsajili Fabregas
kutoka klabu ya Barcelona mapema baada ya kuanza majira ya kiangazi,
licha ya kuwa Asernal ndio walikuwa na uwezekano mkubwa wa kuinasa saini
ya kiungo huyo.
Kitendo cha Fabregas kujiunga Stamford Bridge kiliwashitua wengi kwasababu nyota huyo alikuwa na mapenzi na washika bunduki na aliwahi kuwa nahodha wao.
Fabregas alionesha kuwa Asernal
walimpotezea, lakini Mourinho anadai kiungo huyo kamwe hakutaka kurudi
kaskazini mwa London na alisema ilimchukua dakika 20 tu kumsajili.
"Kwa namna gani nilimshawishi? Nilizungumza naye kwa dakika 20," alisema Mourinho.
"Nadhani kiukweli alikuwa anataka kuja
hapa. Asernal hawakuwa na jinsi na ndio maana hawakuingilia, lakini
sidhani kama alikuwa muwazi kwa hilo. Alikuwa katika uelekeo wetu,
kwahiyo ilikuwa rahisi kwangu.
Maamuzi rahisi: Kocha wa Chelsea amedai ilimchukua dakika 20 tu kumshawishi Fabregas kujiunga Darajani
`The Special One` alizungumzia suala la utata la Wilshere kunaswa akivuta sigara wiki hii.
Kiungo huyo wa washika bunduki alipigwa picha akivuta sigara na kuonesha tabia mbaya wakati wa likizo yake.
Ilikuwa mara ya pili katika miezi tisa, Wilshere kuonekana ana sigara mdomoni, licha ya yeye kujulikana sio mvutaji.
Mourinho alisema kiungo huyo wa England hafanyi kazi yake kama mtu wa kuigwa na jamii baada ya kuendeleza tabia hii.
"Nini wachezaji wa mpira wanafanya,
mamilioni na mamilioni ya watu wanatazama, watoto wengi wanatazama,"
alisema Bosi huyo wa Blues.
"Mimi sio mtaalamu,, lakini sidhani kama
mchezaji anaweza kuathirika kiwango chake kwa kuvuta sigara moja akiwa
na marafiki zake majira ya kiangazi wakati hayuko mazoezini".
"Anayeathirika ni mtoto wa nyumbani, anaanza kuwaza kama mchezaji mkubwa anavuta, nami naweza kuvuta, hakuna tatizo".
Mfano mbaya: Mourinho pia alimmbwatukia Jack Wilshere aliyepigwa picha akivuta sigara wiki hii.
0 maoni:
Post a Comment