Saturday, July 19, 2014


Sabella to decide Argentina future before next week
Imechapishwa Julai 19, 2014, saa 9:07 asubuhi

KOCHA wa Argentina, Alejandro Sabella amesema atafanya maamuzi ya hatima yake ya baadaye ndani ya wikiendi hii.
Kocha huyo mwenye miaka 59 aliiongoza Argentina katika fainali ya kwanza baada ya kupita miaka 24 nchini Brazil na kufungwa bao 1-0 dhidi ya mabingwa Ujerumani.
Sabella ameweka wazi kuwa atafikiria juu ya kazi yake na siku zijazo ataeleza kila kitu,  na kama anataka kuendelea na majukumu yake ataangailia kama ataweza kuhimili mikikimikiki.
“Awali ya yote, sijui mawazo ya AFA (chama cha soka cha Argentina) juu ya hatima yangu, nahitaji kupumzika kwa siku chache. Sitapenda kushikilia sana mambo kwasababu mimi ni mtu wa kuwajibika. Nitalitafakari hili mwishoni mwa wiki hii na nitampigia  simu (Rais wa AFA) Julio Grondona ili tuonane,” aliviambia vituo vya luninga vya C5N na TyC Sports.
“Nitaendelea kuwa kocha kama nitaweza kutoa asilimia 100 ya nguvu zangu, kama ninavyowaomba wachezaji wangu”.
Sabella alisifu mchango wa Lionel Messi katika kampeni za kombe la dunia, akidai kuwa tuzo ya mchezaji bora wa mashindano aliyoipata ilitokana na kiwango chake,  na anadhani alijitolea kadiri awezavyo kuisaidia timu.
“Messi ni mfano wa kile timu ilichofanya. Aliwaza mengi na sio moja, timu ilikuwa juu yake, alitoa kabla ya kupokea”. Alisema Sabella.
“Alijitoa mhanga na kuwa mchezaji bora wa dunia. Alikuwa msaada mkubwa kwetu kufuzu hatua ya kwanza, na alielewa kuwa katika hatua nyingine za mashindano tulitakiwa kubadili mfumo wetu wa uchezaji”.
“Tunajivunia kuwa naye, tunamponggeza Messi kwasababu alijitolea kwa ajili ya timu. Asante kwa kuwa Muargentina, asante kwa kuchagua kuichezea Argentina na asante kwa kuwa tayari kucheza muda wote”.
Sabella aliongeza kuwa bado hajatazama mechi ya fainali aliyofungwa na Ujerumani kwa bao la dakika ya 113 la Mario Gotze, na amekiri kuwa timu yake ilikuwa na nafasi ya kushinda.
“Sijaitazama tena mechi dhidi ya Ujerumani. Nahitaji kupumzika, tungeshinda mechi,” alisema.
“Nawapongeza Ujerumani kwasababu walikuwa ndio timu bora”.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog