Rais
Mpya wa Jumuiya ya Watanzania waliosoma Korea (KAAT), Bw. Stephen
Katemba (Kulia) akizungumza mara baada ya kuchaguliwa. Anayemsikiliza ni
Mwakilishi Mkazi wa KOICA, Bw. Seung-Beom Kim (Kushoto).
Viongozi wapya KAAT na viongozi wa zamani wakipongezana mara baada ya uchaguzi huo.
Makamu
wa Rais wa KAAT aliyemaliza muda wake, Bibi Margaret Alfanies
(Katikati) akizungumza machache mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi
huo. Kushoto ni aliyekuwa Muweka Hazina wa KAAT, Bibi Emilia Maingu na
kulia ni Bw. Stephen Matee ambaye ni Muweka Hazina mpya.
Makamu
wa Rais wa KAAT aliyemaliza muda wake, Bibi Margaret Alfanies (Wapili
Kulia) akikabidhi nyaraka za KAAT kwa uongozi mpya. Kutoka kushoto
pichani ni Bw. Emmanuel Burton (Makamu wa Rais, Tanzania Bara), Bw.
Bukheti Juma (Wapili kushoto) ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar).
Wengine ni Rais Mpya Bw. Stephen Katemba (Katikati) na Bw. Stephen
Matee (Kulia)ambaye ni Muweka Hazina mpya.
Uongozi mpya wa KAAT wakizungumza na Mwakilishi Mkazi wa KOICA, Bw. Seung-Beom Kim (Wapili kulia).
Wakiwa katika picha ya pamoja ni uongozi mpya wa KAAT na baadhi ya viongozi wa zamani wa Jumuiya hiyo.
…………………………………………………………
Na Saidi Mkabakuli
*Wadhamiria kuitangaza Tanzania kibiashara kimataifa
Jumuiya
ya Watanzania waliosoma Korea imefanikiwa kupata uongozi mpya,
utaongoza umoja wa Watanzania hao kwa muda wa miaka miwili.
Waliochaguliwa
kuongoza KAAT ni pamoja na Bw. Stephen Katemba ambaye amechaguliwa kuwa
Rais wa Jumuiya. Bw. Katemba atasaidiwa na Bw. Bukheti Juma (Makamu wa
Rais, Zanzibar) na Bw. Emmanuel Burton (Makamu wa Rais, Tanzania Bara).
Katika nafasi ya Uweka Muweka Haziny
a,
aliyechaguliwa ni Bw. Stephen Matee, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) ulio chini ya Mama Anna Mkapa.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa rasmi jukumu la kuiongoza Jumuiya hiyo, Bw.
Katemba ambaye ni Mtaalamu wa Masuala ya Uchumi na Biashara za
Kimataifa, amesema kuwa Tanzania ina fursa kubwa katika eneo la biashara
za kimataifa kuwa kuzingatia rasilimali zilizopo nchini na kuchagiza
kuwa fursa hizo zinaweza kutumiwa ipasavyo kwa kujitangaza tu.
Bw.
Katemba aliongeza kuwa kama Watanzania tukiwa na uzalendo wa dhati na
kuwa mabalozi wazuri, Tanzania itakuwa na uhakika wa kukamata masoko
makubwa ikiwemo Korea na Bara la Asia kwa ujumla.
“Kwa
mfano kwa mujibu wa hali ya uchumi wa Taifa, kwa mwaka 2013, mwenendo
wa biashara ya bidhaa na huduma nje haukuwa wa kuridhisha
ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2012. Thamani ya mauzo ya bidhaa na
huduma nje ilipungua kwa asilimia 1.7 kutoka Dola za Kimarekani milioni
8,675.6 mwaka 2012 hadi Dola milioni 8,532.0,” alisema.
Kwa
mujibu wa Bw. Katemba kuwa ili kufikia malengo ya kimkakati ya Mpango
wa Maendeleo wa Miaka Mitano ulio chini ya Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango ambao umelenga kufungulia fursa za ukuaji wa uchumi, Tanzania
haina budi kufikia malengo ya kikao cha tisa cha Shirikisho la Biashara
Ulimwenguni (WTO) ambalo linalenga kuziwezesha kibiashara nchi wanachama
kuboresha biashara zao.
“Katika kikao cha tisa cha WTO, Mawaziri wa nchi wanachama 159 wa Shirikisho walikubaliana
kuwa
na “Mpango wa Bali” ambao unalenga kuziruhusu nchi zinazoendelea kuwa
na fursa zaidi ya kuzalisha chakula cha akiba, kuinua kiwango cha
biashara kwa nchi changa na kusaidia maendeleo ya nchi changa
kibiashara. Hivyo, tunaweza kufikia malengo haya kwa kutangaza bidhaa
zetu hasa za vyakula kwa mataifa yenye uhitaji wa bidhaa hizo,”
alifafanua.
Akizungumza
wakati wa mkutano huo, Mwakilishi Mkazi wa KOICA, Bw. Seung-Beom Kim
alisema kuwa Tanzania ina bidhaa nyingi ya kuziuza kwenye soko la Korea
na kutolea mfano mchele wa Kyela kuwa ni bidhaa nzuri kwenye soko hilo.
0 maoni:
Post a Comment