Taifa Stars inayodhaminiwa na bia
ya Kilimanjaro Premieum Lager kesho jumamosi saa 10 kamili kwa saa za
Afrika Mashariki itashuka dimba la Nakivubo kucheza na wenyeji
Uganda.(The Cranes).
Mecho hiyo ya kesho ni mchez wa
marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN mwaka 2016 zitakazofanyika
mapema mwezi Januari nchini Rwanda, mgeni rasmi atakua Rais wa Uganda
Yoweri Mseveni.
Kikosi cha Taifa Stars chini ya
kocha wake mkuu Charles Mkwasa, kiliwasili jijini Kampala jana usiku na
kimefikia katika hoteli ya Grand Global iliyopo jirani na chuo kikuu cha
Uganda Makerere.
Taifa Stars imefanya mazoezi leo
jioni katika uwanja wa Nakivubo yakiwa ni mazoezi mepesi na mwisho
kuzoea uwanja kabla ya mchezo wenyewe utakaofnayika kesho jioni.
Kocha Mkwasa akiongelea kuelekea
mchezo huo amesema, anashukuru vijana wake wamefika salama wote, hali
nzao ni nzuri, morali ni ya hali ya juu, kikubwa wanatambua wana deni
kubwa kwa watanzania hivyo kesho watapambana kuhakikisha wanapata
matokeo mazuri.
Akiongelea hali ya hewa na
mazingira ya timu ilipofikia, Mkwasa amesema hali ya hewa ni ya kawaida
baridi na mvua kidogo haina tofauti sana na Tanzania, mazingira ya
hoteli ni mazuri na kusema kikubwa kilichobaki ni kusaka ushindi katika
mchezo huo na vijana wake wapo tayari.
Wakati huo huo mashabiki zaidi ya
50 kutoka nchini Tanzania wanatarajiwa kuwasili kesho jumamosi alfajiri
wakitokea jijini Dar es salaam kuungana na watanzania wengine waishio
nchini Uganda kuishangilia timu ya Tanzania itakapokuwa ikipimbana na
Uganda katika uwanja wa Nakivubo.
0 maoni:
Post a Comment