Mara nyingi tunasikia stori kuhusu watu
kukamatwa na dawa za kulevya kwenye viwanja vya ndege, wapo wanaotoka TZ
kwenda nje na wapo wanaokamatwa wanaziingiza pia kutoka nje ya nchi..
nina hii stori kutoka ITV kuhusu mtu kukutwa na bangi ndani ya basi.
Basi la Maning’inice
lilitoka Mtwara kwenda Dar, njiani kulikuwa na Checkpoint ya Polisi
ambapo jamaa aliyebeba bangi kwenye begi aliomba akajisaidie, Polisi
walipoingia kwenye gari kukagua wakakutana na begi hilo lililojaa bangi
na jamaa mwenye nalo alikuwa ameshakimbia tayari.
“Kuna mtu
mmoja aliteremka akasema ana mkojo.. Askari akauliza nani mwenye hili
begi yule jamaa akaanza kukimbia vichakani. Askari wakakimbizana nae
maporini, akatokomea“– amesimulia dereva wa basi hilo, Hashim Mohamed.
Bangi iliyokutwa kwenye begi hilo ina
uzito wa kama kilo 25 hivi… Stori hiyo nimeirekodi kwenye Habari
iliyoruka ITV, na haoa utaisikiliza yote kwenye hii sauti.
0 maoni:
Post a Comment