Friday, July 3, 2015



Straika wa Mexico Javier Hernández 'Chicharito' amevunjika mfupa wa begani na kufanyiwa operesheni ambayo itamweka nje kwa Wiki 4 na kukosa kuichezea Nchi yake Mashindano ya CONCACAF Gold Cup.
Chicharito aliumia Jumatano iliyopita huko Houston, USA wakati wa Mechi ya Kirafiki na Honduras iliyoisha 0-0 na kutolewa nje Dakika 5 kabla Haftaimu.
Msimu uliopita, Chicharito, mwenye Miaka 27 na ambae ni Fowadi wa Manchester United, alikuwa na Real Madrid kwa Mkopo na alipaswa kurudi Old Trafford huku kukiwa na fununu za mipango ya kumuuza.

Lakini kuumia kwake na kufanyiwa operesheni iliyomwekea chuma kwenye mfupa wa begani kutamweka nje kwa Wiki 4 na hali hii itafanya mipango hiyo ya Uhamisho wake isitishwe.Kukosekana kwa Chicharito pia ni pigo kwa Mexico kwani ni Mfungaji wa Bao 40 katika Mechi 73 za Nchi hiyo na walimtegemea sana kwenye Mashindano ya CONCACAF Gold Cup ambalo ni Kombe la Mataifa ya Nchi za Marekani ya Kaskazini, ya Kati na Visiwa vya Carribean yakatayochezwa Julai 7 hadi 26 huko Canada na United States.Mexico wako Kundi C na wataanza kwa kucheza na Cuba hapo Julai 9 huko Chicago kisha kuzivaa Guatemala na Trinidad and Tobago.
Kocha wa Mexico Miguel Herrera amemwita Javier Orozco wa Klabu Bingwa ya Mexico Santos Laguna kumbadili Chicharito.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog