KLABU
ya Chelsea imemsajili Radamel Falcao kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu
kutoka Monaco, huku kinda wa Blues, Mario Pasalic akihamia kwa wapinzani
kama sehemu ya makubaliano ya dili hilo.
Mshambuliaji
huyo wa Colombia atacheza Ligi Kuu ya England kwa msimu wa pili akiwa
na kikosi cha Jose Mourinho, baada ya kushindwa kung'ara akiwa na
Manchester United msimu uliopita.
"Nina
furaha sana kujiunga na Chelsea na nina hamu ya kuanza mazoezi na
kusaidia dhamira yetu ya kutetea ubingwa na kupata mafaniko Ulaya,"
amesema Falcao.
Kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois akiokoa dhidi ya Radamel Falcao msimu uliopita; wawili hao sasa wanaungana London
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 29, aliitua Old Trafford msimu uliopita kama
mmoja wa washambuliaji tishio Ulaya, lakini maumivu ya goti aliyoyapata
wakati anacheza Monaco yalionekana kumpunguza makali.
Kinda
Mcroatia, Pasalic, ambaye msimu uliopita alikuwa kwa mkopo Elche katika
La Liga, sasa atakwenda kwa mkopo Monaco kama sehemu ya dili hilo.
Falcao
ataungana na Diego Costa, Thibaut Courtois na Filipe Luis, ambao wote
wamewahi kuchezea Atletico Madrid, sambamba na mchezaji mwenzake wa
kimataifa wa Colombia, Juan Cuadrado Uwanja wa Stamford Bridge.
0 maoni:
Post a Comment