Tuesday, November 3, 2015


Former Lyon manager Remi Garde has emerged as the early favourite with the bookmakers and held talks with Newcastle last season Aston Villa watamteua mkufunzi wa zamani wa Lyon Remi Garde kuwa kocha wao mpya leo, kujaza nafasi ya Tim Sherwood aliyefutwa kazi.
Mfaransa huyo atatia saini mkataba wa miaka mitatu unusu na atafuatilia mechi ya Jumatatu dhidi ya Tottenham ugenini kutoka eneo wanamoketi mashabiki.
Mkufunzi huyo wa miaka 49 anachukua klabu hiyo ikiwa inashika mkia Ligi ya Premia baada ya kushinda alama nne pekee kutoka kwa mechi 10.

Kocha wa Bastia Reginald Ray ndiye atakayekuwa msaidizi wa Garde na wawili hao watasimamia mechi yao ya kwanza nyumbani dhidi ya Manchester City Jumapili ijayo.
Garde alisaidia Lyon kumaliza nambari nne, tatu na tano katika misimu mitatu aliyokuwa nao kuanzia 2011 kabla ya kuwaacha 2014 kutokana na sababu za “kibinafsi na kifamilia”.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog