Thursday, September 17, 2015


Mkuu wa mauzo na masoko wa GSM Media, Elibariki Lukumay,(kulia) akimkabidhi mfano wa hundi Mwenyekiti wa Chama cha Wandishi wa Michezo (TASWA) Juma Pinto kwa ajili ya kumuaga Rais Kikwete pamoja na tuzo kwa wanamichezo zitakazofanyika Oktoba 8, Mlimani City, Dar es Salaam. Katikati ni M/Mkiti wa TASWA, Egbert Mkoko. (Picha na Rahel Pallangyo)

Mkuu wa mauzo na masoko wa GSM Media, Elibariki Lukumay akizungumza wakati wa mkutano na wandishi wa habari, Kulia ni Katibu wa TASWA, Amir Mhando na Katikati ni Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto
KAMPUNI ya GSM Media ya Dar es Salaam imetoa Sh milioni 50 kwa ajili ya kudhamini tuzo za wanamichezo waliofanya vizuri zaidi katika miaka 10 ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.
Utoaji wa tuzo hizo utafanyika Oktoba 8, mwaka huu ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, ambapo wanamichezo pia watatumia tuzo hizo zilizoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kumuaga Rais Kikwete anayemaliza muda wake kikatiba.
Kwa mujibu wa TASWA licha ya kumuaga Rais Kikwete na kutoa tuzo kwa wanamichezo 10 waliofanya vizuri zaidi, pia chama hicho kitatoa Tuzo ya Heshima Rais Kikwete ikiwa ni kuthamini mchango wake kwa michezo katika utawala wake. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kutambulisha udhamini huo Dar es Salaam jana, mwakilishi wa GSM Foundation, Elibariki Lukumay, alisema wameguswa na tukio hilo na kuona kuna umuhimu wa kuiunga mkono TASWA.

“Taasisi yetu ambayo ina kampuni mbalimbali imeguswa na kitendo ambacho TASWA inakiandaa na kwa kuanzia tunatoa kiasi hicho cha fedha kufanikisha jambo hilo na tunawaomba wengine pia waunge mkono.

“Rais Kikwete amefanya mambo makubwa katika michezo nchi hii, hivyo tukiwa pia wadau wakubwa wa michezo tumeona ni vyema tuungane na wenzetu wa TASWA katika kumuaga na kumshukuru kwa mchango mkubwa alioufanya kwa michezo,” alisema Lukumay.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto aliishukuru taasisi hiyo na kusema kuwa bajeti ya tukio hilo ni Sh milioni 130 na kwamba wadhamini hao wamefungua milango kwa wengine ili kulifanikisha jambo hilo.

“Tunaamini mchango wa Rais Kikwete katika medani ya michezo hauna mfano na kila mdau wa michezo atakubali amefanya mambo makubwa kwa michezo.
“Tunafahamu Rais alivyosimamia serikali yake kulipia makocha wa michezo ya soka, netiboli na ngumi. Pia chini ya utawala wake serikali ilipeleka wanariadha wetu China, Ethiopia na New Zealand kwa maandalizi ya mashindano ya kimataifa,” alisema.

Alifafanua kuwa karibu vyama vyote vya michezo nchini vitashikirikishwa katika tukio hilo ikiwa ni pamoja kuwa karibu kwa kila hatua na Wizara Ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog