KOCHA mpya wa Real Madrid, Rafael Benitez ataonja joto ya pambano la watani Hispania, maarufu kama El Clasico wakati Los Blancos watapokutana na Barcelona kwa mara ya kwanza mechi ya mzunguko wa kwanza wa La Liga Novemba 8 Uwanja wa Bernabeu.
Mechi
ya marudiano baina ya miamba hao walioweka kwenye 'viganja vyao' soka
ya Hispania itafanyika April 3 mwakani, Uwanja wa Camp Nou.
Kocha
Luis Enrique aloyeshinda mataji matatu na Blaugrana msimu uliopita,
ataanzia kampeni yake ugenini kwa kumenyana na Athletic Bilbao Agosti 23
- mechi ya tatu ya wiki baina yao baada ya kikosi cha Ernesto Valverde
kumenyana nao Barca mara mbili katika mechi za Super Cup.
Lionel Messi alifunga katika mechi ambayo Barcelona iliifunga Atletico Madrid kujihakikishia taji la La Liga msimu uliopita
Benitez
yeye ataanza kampeni yake msimu huu kwa kumenyana na Sporting Gijon
Uwanja wa El Molinon katika siku ya ufunguzi, wakati Malaga
itaikaribisha Sevilla Uwanja wa La Rosaleda katika mechi ya mahasimu wa
Andalucian.
Katika
siku ya mwisho ya msimu wa 2015-2016, Mei 15, Real itasafiri hadi
Galicia kuwafuata Deportivo La Coruna, wakati Barcelona pia watamalizia
ugenini dhidi ya Granada, ambao walishika nafasi ya 17 katika msimu
uliopita wa La Liga.
Kikosi
cha Diego Simeone, Atletico Madrid chenyewe kitaanzia msimu mpya wa La
Liga nyumbani wakiwakaaribisha Las Palmas na kumalizia nyumbani kwa
Celta Vigo.
Atletico,
ambayo msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya tatu ikiwa inazidiwa
pointi na 16 na Barcelona, itamenyana na Real Madrid Uwanja wa Vicente
Calderon Oktoba 4 na baadaye marudiano Uwanja wa Bernabeu, Februari 28
0 maoni:
Post a Comment