Tuesday, March 10, 2015



Mshindi wa tatu wa Miss Tanzania 2014,Doris Mollel akishiriki zoezi la uchangiaji damu katika ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya wanawake Duniani,iliyofanyika Buguruni Chama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto Ofisa Muuguzi kutoka Benki ya Damu Salama,Selina Joseph. Zoezi hilo la uchangiaji damu liliandaliwa na Mrembo huyo. 

Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani,mrembo Doris Mollel ambaye ni Miss Tanzania namba tatu kwa mwaka 2014 ameongoza mamia ya watanzania katika zoezi la kizalendo la kuhamasisha kuchangia damu kwa watanzania kwa ajili ya wagonjwa mbalimbali,zoezi ambalo limefanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. 

Zoezi hilo ambalo lilikuwa linaongozwa na mpango wa taifa wa damu salama kwa udhamini wa kampuni ya METL lilikuwa na lengo la kupata damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya Mama na Mtoto kwani matatizo ya damu katika hospitali za Tanzania yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku,jambo lililompelekea mrembo huyo kuamua kujitoa kuhamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo. 

Zoezi hilo lilifanyika Machi 8 mwaka huu katika maeneo ya Buguruni Chama kwa muda wa siku nzima,ambapo jumla ya uniti 65 za damu zimepatikana kiwango ambacho kimetajwa kuwa kinatia matumaini kwa mrembo huyo kufanikiwa katika kuwahamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi. 
Akizungumza na wanahabari kuhusu kitu kilichomsukuma kuendesha zoezi hilo,Doris alisema kuwa ameamua kufanya hivyo baada ya kugundua kuwa wakina mama wengi pamoja na watoto hufariki dunia wakati wa kujifungua kutokana na kukosa damu ya kuongezewa,jambo ambalo amesema ni lazima watanzania kuungana kwa pamoja kutafuta damu ya kutosha katika kila hospitali ili kuiondoa hali hiyo ambayo inaweka hatarini maisha ya mama na mtoto wa kitanzania. 

Amesema kuwa swala la kujitolea damu ni swala la kizalendo zaidi na moyo wa kujitoa kwa kuwa kila mtanzania anaweza kuwa na uhitaji wa damu muda wowote hivyo ni lazima watanzania wawe na utamaduni wa kuchangia damu mara kwa mara kwani itasaidia endepo kutatokea uhitaji wa damu katika mahospitali yetu.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog