Wanawake wa mgodi wa
Acacia Buzwagi kupitia mfuko wa maendeleo wa mgodi huo wameshiriki siku
ya wanawake kwa kutoa misaada mbalimbali kwenye vituo viwili vya
kulelea watoto yatima wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Wanawake hao kupitia kwa
makamu meneja wa Acacia Buzwagi Simon Sanga wamekabidhi Misaada hiyo
katika vituo vya kulelea watoto yatima vya Muvuma kilichopo Nyasubi
pamoja na kituo cha Peace Orphanage Center kilichopo mtaa wa Nyihogo.
Akikabidhi misaada hiyo
makamu meneja wa Acacia Buzwagi Simon Sanga amesema wameamua kutoa
misaada hiyo kwa kutambua uwepo wa jamii inayozunguka mgodi na kuongeza
kuwa wataendelea kushirikiana na jamii ikiwa ni moja ya wajibu wao
kuwasadia wananchi.
Wakipokea misaada hiyo
kwa nyakati tofauti viongozi wa vituo hivyo wameshukuru Acacia Buzwagi
kwa kutambua uwepo wa watoto yatima ambao wanahitaji misaada toka kwa
wananchi na wadau mbalimbali wanaoguswa na makundi yasiyojiweza katika
jamii wakiwemo yatima.
Picha ya Pamoja ya wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi na watoto Yatima.
Naye mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima Muvuma Jacquline Pius
kwa niaba ya wenzake amewashukuru wanawake wa Acacia Buzwagi kwa
kujitoa na kuwakumbuka na amewakaribisha kushiriki katika masuala
mengine katika kituo hicho.
Wafanyakazi wa Buzwagi wakishiriki michezo mbalimbali na watoto hao.
Pia kuna picha za
chakula cha pamoja cha mchana na watoto hao,,kuna picha pia za michezo
mbalimbali ambazo wafanyakazi wa Mgodi wa Acacia walishiriki michezo
hiyo na watoto yatima
0 maoni:
Post a Comment