Rooney, Miaka 28, anachukua wadhifa uliokuwa ukishikiliwa na Nemanja Vidic ambae amemaliza Mkataba wake na kuhamia Inter Milan Mwezi uliopita.
Klabu hiyo pia imemteua Darren Fletcher kuwa Msaidizi wa Rooney.
Jana, wakicheza Mechi ya Kirafiki na Valencia Uwanjani Old Trafford na kushinda 2-1, Rooney ndie alivaa utepe wa Nahodha na Jumamosi Agosti 16 ataiongoza Man United hapo hapo Old Trafford kwenye Mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England Msimu mpya wa 2014/15 dhidi ya Swansea City.
Akiongea baada ya kuteuliwa, Rooney alisema: “Hii ni heshima kubwa mno na nitatumikia kwa fahari kubwa. Namshukuru sana Meneja kwa imani yake aliyoonyesha kwangu.”
Rooney, alieanzia Soka lake huko Everton, ameshawahi kuwa Nahodha kwenye Mechi kadhaa huko nyuma.
Akiwa na Man United, Rooney ameshatwaa Ubingwa wa England mara 5, UEFA CHAMPIONS LIGI Mwaka 2008 na hivi sasa anashika Nambari 3, nyuma ya Sir Bobby Charlton na Denis Law, katika Ufungaji bora wa Magoli katika Historia ya Man United akiwa na Mabao 216.
Ingawa wengi walitarajia Meneja Louis van Gaal atamteua Robin van Persie kuwa Nahodha hasa kwa vile ndie alikuwa Nahodha wa Netherlands wakati Van Gaal akiwa Kocha Mkuu wa Nchi hiyo na urahimu na ukaribu wao, Meneja huyo amemchukua Rooney kutokana na kuwa Mchezaji mzoefu wa muda mrefu hapo Old Trafford.
Rooney alijiunga na Man United Mwaka 2004.
Akiongelea uteuzi huu, Van Gaal alisema: “Kwangu mimi ni muhimu sana uchaguzi wa Kepteni. Wayne ameonyesha mfano mzuri sana kwa kila analofanya. Nimevutiwa sana na kazi yake na ari yake Mazoezini na kwenye falsafa yangu.”
Kabla ya Nemanja Vidic kuwa Nahodha, Gary Neville ndio alioshika wadhifa huo na Wakongwe wengine, ambao ni Malejendari, walioshika Nafasi hiyo ni kina Sir Bobby Charlton, Bryan Robson, Eric Cantona na Roy Keane
0 maoni:
Post a Comment