Wednesday, August 13, 2014


Cristiano Ronaldo, Jana alipiga Bao zote 2 wakati Real Madrid inaichapa 2-0 Sevilla na kutwaa UEFA Super Cup huko Cardiff, Wales na kumfanya afikishe Bao 70 katika Mashindano ya Ulaya na hivyo kumpiku Lionel Messi katika Ufungaji.
Mwezi Aprili 2012, Ronaldo alikuwa Bao 18 nyuma ya Messi kwa Ufungaji Mabao kwenye Mechi za Klabu Barani Ulaya lakini tangu wakati huo Ronaldo alicharuka na kupiga Bao 12 Msimu wa Mwaka huo na kisha kuweka Rekodi ya kufunga Bao 17 kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu uliopita na Bao zake 2 za Jana zimemfanya ampite Messi kwa Bao 2.

Hivi sasa Ronaldo ana Bao 70 kwa Mechi za Ulaya na kufungana na Straika wa zamani wa AC Milan na Juventus, Filippo Inzaghi, na wote kukamata Nafasi ya Pili ya Ufungaji Bora Ulaya katika Historia.
Real Madrid
Ronaldo sasa amebakisha Bao 6 tu kumkamata Mfungaji Bora Ulaya wa Kihistoria, Raul, aliekuwa akichezea Real Madrid, mwenye Bao 76 alizofunga akiichezea Real na Schalke.
Hadi sasa, Ronaldo ameifungia Real Bao 254 katika Mechi 247.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog