Moto Mkubwa ukiendelea kuwaka
katika eneo la juu la Jengo la Shule ya Sekondari ya Kiislam ya Mivumoni
(Mivumoni Islamic Seminary) iliyopo ndani ya Msikiti wa
Mtambani,Kinondoni B Jijini Dar es Salaam jana.
Eneo hilo ambalo lilikuwa likitumika
kama Mabweni ya Wanafunzi wa Shule hiyo,Maabara na Ofisi za Walimu
limeteketea kabisa kiasi kwamba hakuna kitu chochote kilichoweza
kuokolewa.
Jitihada za kuuzima moto huo
zimekuwa zikiendelea hadi hivi sasa,huku sehemu ya Waumini wa Kiislam
wakijitokeza kwa wingi kusaidia juhudi hizo za kuuzima moto huo
zilizokuwa zikiendesha na Kampuni ya Kuzima moto ya Ultimate,japo baadae
gari hilo liliisha maji,hali iliyowapelekea Waumini hao kulijaza maji
gari hilo kwa kurumia ndoo huku kazi ya Uzimaji moto huo ikiendelea.
Chanzo cha Moto huo,inadaiwa ni
hitilafu ya Umeme iliyokuwepo kwenye Bweli la Wasichana Wanafunzi wa
Shule hiyo.Hakuna mtu yeyote aliepoteza maisha wala kujeruhiwa katika
tukio hilo.Picha zote na Othman Michuzi.Kwa hisani ya http://issamichuzi.blogspot.com/
Moto mkubwa ukiendelea kuwaka kwenye eneo hilo.
Ulinzi mkali wa Polisi ulitawala katika eneo la Msikiti huo wa Mtambani kuhakikisha Usalama unakuwepo kwenye eneo hilo.
Baadhi ya Waumini wa Kiislam wakishirikiana kusombelea maji ili kuuzima moto huo.
Gari la Zima Moto mali ya Kampuni ya Ultimate Security likijazwa maji kwa ndoo ili kuendelea na zoezi la uzimaji w amoto huo.
Likafika na gari hili kwa ajili ya kusaidia kuzima moto huo.
0 maoni:
Post a Comment