Mahakama ya kikatiba nchini
Uganda imefutilia mbali sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ambayo
ilisababisha mataifa ya magharibi kuinyima msaada.
Kadhalika sheria hiyo ilizua gumzo sana sio tu
Uganda bali kote duniani ambapo mataifa ya Magharibi yalilazimika
kuingilia kati. Mahakama ilisema kuwa mswada huo kabla ya kuidhinishwa kuwa sheria ulipitishwa na wabunge ambao idadi yao haikutosha kupitisha mswada na kwa hivyo ni kinyume na sheria.
Mataifa kadhaa ya Magharibi yamesitisha msaada kwa Uganda hasa baada ya sheria hiyo mpya kupitishwa.
0 maoni:
Post a Comment