Friday, August 1, 2014


France training in Kiev's Olympic Stadium last year


UEFA imethibitisha kuwa itachunguza tatizo la mashabiki kuvamia uwanja katika mechi ya kufuzu ligi ya mabingwa barani Ulaya baina ya Copenhagen na Dnipro Dnipropetrovsk.
Kipindi cha pili katika mechi  hiyo ya kwanza ya raundi ya tatu iliyopigwa uwanja Kiev Olympic ilisimama kwa dakika 10 baada ya mashabiki wageni kutoka Uholanzi kuingia uwanjani wakijihami kushambuliwa na kundi lingine, ambalo limeripotiwa kuwa mashabiki wa Dnipro.
Timu hizo mbili zilikuwa zimeingia uwanjani kuanza kipindi cha pili, lakini zilirudi tena kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakati maaskari wakijaribu kuwatoa mashabiki wa Ukraine waliovamia mashabiki wageni ndani ya uwanja.
Baada ya wana Usalama kufanikiwa kuwatoa, mechi iliendelea kama kawaida.
Mkurugenzi mkuu wa Copenhagen, Anders Horsholt aliwalaumu Dnipro na uongozi wa uwanja kwa kushindwa kuimarisha ulinzi na taarifa kwa vyombo vya habari kutoka UEFA inaeleza kuwa mamlaka inayohusika itafanya uchunguzi wa tukio hilo.
“Uchunguzi imeanza dhidi ya mashabiki wa Dnipro Dnipropetrovsk na kutojipanga kwa ulinzi,” Taarifa ilisomeka.

Mashabiki wa Dnipro wameripotiwa wakilaumu  kuwa mashabiki wageni walinyanyua bendera ya Urusi katika eneo lao kuwakebehi wanyeji, lakini taarifa ya Copenhagen kwenye tovuti yake rasmi imekanusha tuhuma hizo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog