DIEGO Lopez yupo tayari kuondoka Real Madrid
majira haya ya kiangazi kwasababu ya kukosa namba ya kudumu katika kikosi cha
kwanza.
Kipa huyo mwenye miaka 32 alijiimarisha chini ya
Carlo Ancelotti aliyependelea kumuanzisha katika mechi za La Liga msimu uliopita,
lakini alipoteza nafasi hiyo kwa kipa mwenzake Iker Casillas aliyekuwa
anapangwa zaidi katika mechi za kumalizia msimu.
Kwa wiki kadhaa sasa, Madrid wanaiwinda saini ya
kipa wa kimataifa wa Costa Rica, Keylor Navas na dili hilo litakamilika
jumatatu baada ya rais wa Real Madrid, Florentino Perez kuwaomba Levante
wacheleweshe uthibitisho mpaka kikosi kitakapokuwa kimerudi nchini Hispania
kutoka katika kambi ya maandalizi ya msimu nchini Marekani.
Vyanzo vya habari vinasema, Lopez anaweza kuwa
kipa namba tatu msimu ujao kwasababu watakuwepo makipa watatu wa kiwango cha
juu.
Na ndio maana anataka kuondoka Santiago Bernabeu
na anatarajia kuzungumza na Real Madrid baada ya kujua wapi pa kwenda.
Ancelotti ameshafikia maamuzi ya kumtumia kipa wa
kimataifa wa Hispania, Iker Casillas kama chaguo la kwanza msimu ujao licha ya
makosa aliyokuwa nayo msimu uliopita kwenye mechi ya nusu fainali ya ligi ya
mabingwa na fainali za kombe la dunia nchini Brazil.
Muitaliano huyo hataki tena kubadilishabadilisha
makipa kama alivyofanya msimu uliopita, hivyo nafasi ya Lopez inaonekana kuwa
ndogo zaidi.
0 maoni:
Post a Comment