Friday, August 1, 2014


Chelsea boss Mourinho hints at Cech exit

JOSE Mourinho ameweka wazi kuwa kipa namba moja wa muda mrefu wa Chelsea, Petr Cech anaweza kuondoka klabuni hapo majira haya ya kiangazi mwaka huu.
Baada ya Thibaut Courtois kurejea klabuni kutokea klabu ya Atletico Madrid alipokuwa anacheza kwa mkopo, tetesi zimeshaanza kuzuka kama kipa wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech ataendelea kushikilia namba moja katika dimba la Stamford Bridge.
Mtandao wa Goal unafahamu kuwa Chelsea wapo tayari kusikiliza ofa kutoka klabu ya PSG iliyoonesha nia , na Mourinho amesema Cech anaweza kuondoka kwa kutegemea Mark Schwarzer kuwa kipa namba mbili.
“Petr yupo tayari kupigania nafasi yake, lakini Thibaut ni kipa bora zaidi kijana duniani, hakuna wasiwasi juu ya hilo,” Kocha huyo Mreno alikaririwa akizungumza na Evening Standard.
“Watachuana na kwangu mimi ni tatizo zuri la kufanya maamuzi.
“Sisi ti timu inayohitaji kuwa imara na kushindania makombe na tunahitaji ushindani wa nafasi.
Courtois amerudi klabuni baada ya kuonesha kiwango kizuri akiwa na timu ya taifa ya Ubelgiji na amesisitiza kuwa anahitaji kutengeneza jina nchini England kama alivyofanya Hispania.

“Nilisaini mkataba hapa miaka mitatu iliyopita, kwasasa nina furaha ya kuwa hapa, kuwa sehemu ya klabu,” aliiambia Tovu rasmi ya Chelsea.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog