Friday, August 1, 2014


Official: Malaga swoop for Ochoa


MALAGA imetangaza kumsajili kipa Guillermo Ochoa ili arithi mikoba ya Willy Caballero.
Kipa huyo mwenye miaka 29, raia wa Mexico,  alikuwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na klabu ya Ajaccio kumalizika mwishoni mwa msimu uliopita na alikuwa na ofa nyingi kufuatia kuonesha kiwango cha ajabu katika fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil.
Ochoa ameamua kusaini Malaga ambao walikuwa wanatafuta kipa namba moja baada ya Caballero kujiunga na Manchester City.
Malaga walitangaza jana jioni kuwa kipa huyo atatangazwa rasmi kwenye mkutano na waandishi wa habari majira ya saa 11:00 jioni kwa saa za Hispania.

Ochoa aliyeichezea nchi yake mechi 63, alianza maisha yake ya soka huko America kabla ya kujiunga na Ajaccio mwaka 2011.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog