Friday, August 29, 2014
1:41 AM
Unknown
UEFA Leo imempa Tuzo yao ya Mchezaji Bora wa Mwaka Cristiano Ronaldo baada ya kuwabwaga kwenye Kura Kipa wa Mabingwa wa Dunia Germany, Manuel Neuer na Mchezaji mwenzake wa Klabu ya Bayern Munich anaechezea Holland, Arjen Robben.
Ronaldo, Miaka 29, alifunga Bao 17 katika Mechi 11 za Ulaya wakati Real Madrid inaelekea kutwaa Taji lao la 10 la Ulaya walipobeba Kombe la UEFA CHAMPIONS LIGI na pia kuisaidia Klabu yake kutwaa Copa del Rey Msimu uliopita huko Spain.
Baada ya kukabidhiwa Tuzo yake, Ronaldo alisema: “Nimefurahi kweli kweli. Lazima niwashukuru Wachezaji wenzangu, Familia yangu, Marafiki zangu. Sina Kombe hili kwenye Makumbusho yangu, nitaliweka!”
Awali Majina ya Wachezaji 35 yalipigiwa Kura na kubakia 10 na kutangazwa hapo Julai 18 na kisha kubakishwa Matatu ambayo hii Leo ndio Mshindi kapatikana.
Wapigaji Kura ya Tuzo hii ni Jopo la Wanahabari maalum toka Nchi zote Wanachama wa UEFA.
Tuzo hii ilianzisha na UEFA Mwaka 2011 ili kuziba pengo la Ballon d'Or ambayo iliunganishwa na Tuzo ya FIFA ya Mchezaji Bora Duniani na pia kuibadili ile Tuzo ya zamani ya UEFA ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Klabu.
WASHINDI WALIOPITA:
2010–11 Lionel Messi [Barcelona]
2011–12 Andrés Iniesta [Barcelona]
2012–13 Franck Ribéry [Bayern Munich]
1:37 AM
Unknown
DROO
ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI imefanyika leo hii usiku huko Monaco na
Timu 4 za England, Manchester City, Liverpool, Chelsea,na Arsenal zimepata timu za kucheza nazo.
Taswira huko MonacoRonaldo Mchezaji Bora 2014 Ulaya.Ronaldo akibusu tuzo yake yake baada ya kuchaguliwa mchezaji boraRonaldo amewabwaga chini wachezaji wa Bayern Munich kipa Manuel Neuer na Arjen RobbenMchezaji wa zaani wa Real madrid captain Fernando Hierro akionesha karatasi ya kuonesha City Kundi E kundi ambalo linaonekana gumu.
Kipa wa Spain Iker Casillas alionesha Chelsea kwenye kundi G
Droo ya UEFA Champions League ni kama ifuatavyo:-
DROO YA MAKUNDI - UEFA CHAMPIONS
Kundi A: Atletico Madrid, Juventus, Olympiakos, Malmo
Kundi B: Real Madrid, Basel, Liverpool, Ludogorets Razgrad
Kundi C: Benfica, Zenit St Petersburg, Bayer Leverkusen, Monaco
Kundi D: Arsenal, Borussia Dortmund, Galatasaray, Anderlecht
Kundi E: Bayern Munich, Manchester City, CSKA Moscow, Roma
Kundi F: Barcelona, Paris St-Germain, Ajax, APOEL Nicosia
Kundi G: Chelsea, Schalke, Sporting Lisbon, Maribor
Kundi H: Porto, Shakhtar Donetsk, Athletic Bilbao, BATE Borisov
1:37 AM
Unknown
KEPTENI wa Manchester United Wayne Rooney ndie ameteuliwa Nahodha mpya wa England na Meneja wa Timu Roy Hodgson.
Rooney, mwenye Miaka 28, anachukua wadhifa huo kutoka kwa Steven Gerrard wa Liverpool ambae amestaafu kuichezea England mara baada ya Nchi hiyo kutolewa hatua ya Makundi ya Fainali za Kombe la Dunia Mwezi Juni huko Brazil.
Rooney ameichezea England mara 95 na kufunga Bao 40 na Mwezi uliopita aliteuliwa kuwa Nahodha wa Manchester United na Meneja Louis van Gaal.
Mechi za kwanza kwa Rooney kama Nahodha wa England hapo Septemba 3 wakati England itacheza Mechi ya Kirafiki na Norway Uwanjani Wembley na kisha Septemba 8 kusafiri kwenda kucheza na Uswisi katika Mechi yao ya kwanza ya EURO 2016.
Mara baada ya kuteuliwa Rooney, Meneja Roy Hodgson alitangaza Kikosi chake cha England chenye Wachezaji wapya Wanne.
Wapya hao nI beki wa Arsenal mwenye Miaka 19, Calum Chambers, Mchezaji wa Newcastle Jack Colback, Danny Rose wa Tottenham na Fabian Delph wa Aston Villa, wote wakiwa na Umri wa Miaka 24.
KIKOSI CHA ENGLAND:
Makipa: Fraser Forster (Southampton), Ben Foster (West Bromwich Albion), Joe Hart (Manchester City)
Mabeki: Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Calum Chambers (Arsenal), Phil Jagielka (Everton), Phil Jones (Manchester United), Danny Rose (Tottenham Hotspur), John Stones (Everton)
Viungo: Jack Colback (Newcastle United), Fabian Delph (Aston Villa), Jordan Henderson (Liverpool), James Milner (Manchester City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal) Raheem Sterling (Liverpool), Andros Townsend (Tottenham Hotspur), Jack Wilshere (Arsenal)
Mafowadi: Rickie Lambert (Liverpool), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool), Danny Welbeck (Manchester United)

1:32 AM
Unknown
Emanuel Okwi wa Uganda ambaye msimu uliopita alikuwa anaichezea Yanga,
akiwa na jezi namba 25 aliyokabidhiwa mara baada ya kusaini tena Simba
baada ya kukachwa na Yanga katika usajili wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara inayotarajia kuanza mwezi ujao.
Yametimia, hatimaye Emmanuel Okwi amerejea katika kikosi chake cha zamani cha Simba.
Okwi rasmi anasaini leo kujiunga na Simba baada ya kuelewana na uongozi wa klabu hiyo.
Mganda huyo amechukua uamuzi wa kusaini kuichezea Simba baada ya Yanga kumtema.
Okwi rasmi anasaini leo kujiunga na Simba baada ya kuelewana na uongozi wa klabu hiyo.
Mganda huyo amechukua uamuzi wa kusaini kuichezea Simba baada ya Yanga kumtema.
Thursday, August 28, 2014
7:45 AM
Unknown
Toka
nimeanza kuandika na kufatilia habari sijawahi kusikia jeshi la nchi
limechukua hatamu kuendesha mashindano ya urembo tena mashindano
yanayokutanisha warembo kutoka sehemu mbalimbali za taifa ili kumtafuta
mshindi.
Stori
hii ya kipekee inatokea Uganda ambapo jeshi la nchi hiyo limeamua hivyo
baada ya kuona ubabaishaji unaofanywa na Waandaaji wa Miss Uganda
shindano ambalo halikufanyika kwa miaka kadhaa kutokana na ubabaishaji.
Ripota wa TZA Kampala
Bill the African, ameripoti kwamba mmoja kati ya wenye vyeo vyao
jeshini ambae pia ni mdogo wake Rais Museven amesema jeshi limeamua
kuchukua usimamizi wa mashindano haya kwa madai kwamba ni njia ya
kuwavutia vijana wapende kilimo kitakachotangazwa kupitia haya
mashindano ikiwa tayari pia jeshi hilo limechukua Wizara ya kilimo kwa
ajili ya kuiongoza.
Bill
alipozunguka mtaani kuwauliza watu maoni yao imekua 30 kwa 70 yani kuna
ambao wanaona hakuna shida Wagumu hawa kuongoza mashindano hayo lakini
wengine wengi wanapinga wakisema Jeshi hili linajulikana kabisa huwa
halicheki na mtu wala halina urafiki na Raia sasa ndio wataweza
kuendesha mashindano ya Urembo? ni vitu viwili tofauti kabisa.
7:41 AM
Unknown
Siku
kadhaa baada ya Frank Lampard kutangaza kustaafu soka la kimataifa –
jana ilikuwa siku nyingine kwa wanasoka wawili wa kimataifa barani nao
walitangaza uamuzi wa kuachana na soka la kimataifa.
Samuel Eto’o na Xabi Alonso kwa wakati tofauti jana walitumia
mitandao ya kijamii kutangaza uamuzi wao wa kuachana na soka la
kimataifa.
Alianza Xabi Alonso kupitia mtandao wa Twitter kutangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Spain.
Kiungo huyo wa Real Madrid ameshaitumikia Spain kwa muda wa miaka 11 na ameifungia nchi hiyo magoli 16 katika mechi 114.
Wakati huo huo mfungaji mabao mengi zaidi wa timu ya taifa ya Cameroon Samuel Eto’o ametangaza kustaafu soka la kimataifa.
Mshambuliaji huyo ambaye ameifungia Cameroon mabao 56 amejiunga na Everton ya Uingereza juzi .
Kufuatia kauli hiyo mshambuliaji huyo sasa hatakuwepo katika kipindi chote cha cha kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwezi Januari mwakani.

7:38 AM
Unknown
Wiki kadhaa baada ya kuteuliwa kuwa nahodha mpya wa Manchester
United, mshambuliaji Wayne Rooney leo amepata uongozi mpya kwenye medani
za soka.
Rooney ameteuliwa na kocha Roy Hodgson amemteua mshambuliaji huyo kuwa nahodha mpya wa timu hiyo ya taifa.
Rooney mwenye miaka 28 amechukua mikoba iliyoachwa na kiungo wa Liverpool, Steven Gerrard aliyestaafu.
Rooney aliwahi kuvaa kitambaa cha unahodha akiiongoza England kwenye mechi ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia dhidi ya San Marino, Oktoba 2012.
Staa huyo amewapiku wachezaji wenzake kipa Joe Hart na beki Gary Cahill ambao nao walikuwa wakitajwa kuchukua uongozi huo.

2:44 AM
Unknown
- Serengeti fiesta Moshi wapewa fursa ya kuonja radha
Mhehimiwa Temba ametangaza rasmi kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la “Wazee
wa jiji” jumamosi hii. Serengeti fiesta Moshi wamepewa fursa ya kuonja
radha ya wimbo huo siku ya Jumamosi katika uwanja Majengo Jijini humo.
Mheshimiwa Temba ambaye ni mzawa wa jiji
hilo anatarajia kutumia fura ya Serengeti fiesta Moshi kuuzindua wimbo
huo kwa mara ya kwanza.
“Ni matumaini yangu kuwa Wanamoshi
wataniunga mkono kwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja wa Manjengo
siku ya Jumamosi Agosti 30, kushuhudia shoo kali nitakayoifanya sanjari
na nyota wengine wa muziki watakaotumbuiza katika tamasha hilo.
Baadhi ya wasanii watakaowasha moto
katika jukwaa la Serengeti fiesta Moshi ni pamoja na Ali kiba, Ney
waMitego, Dully Sykes, Jambo Squad, Stamina, Maua, Recho, Shaa and
Mapacha, Chege na Temba na wengine wengi.
Chege ameishukuru kampuni ya Serebgeti
kupitia kinyaji chake mashuhuri, Serengeti Premium Lager, kwa kutoa
fursa kwa wasanii kukutana na mashabiki zao na kuwapa burudani.
“Burudani la Serengeti fiesta ni moja ya mifano dhahiri inayoonyesha
jinsi Watanzania tunavyopendana bila kujali utofauti wa makabila yetu na
dini zetu.”
Temba ameyashauri makampuni mengine
yanayopatikana ukanda wa Afrika Mashariki na kati kuiga mfano wa
Serengeti Fiesta ili kudumisha udugu na ujamaa katika nchi wanazofanya
kazi.
Pia ameishauri kampuni ya Serengeti
fiesta kuangalia uwezekano wa kulisambaza burudani hili katika nchi
nyingine Africa…ikianzia na Afrika ya Mashariki.
“Burudani inanguvu ya kipekee sana katika
maisha ya manadamu. Kwa kuisambaza Serengeti fiesta katika nchi
nyingine Afrika mashariki kutaifanya jumuia hii kuungana zaidi na kuwa
kitu kimoja,” alisema Temba.
Baada ya Mohi, Burudani la Serengeti
fiesta litaelekea mikoa mingine kama Musoma, Shinyanga, Kigoma, Tabora,
Singida, Dodoma, Moshi, Arusha, Mtwara na baadae jijini Dar es salaam.
2:30 AM
Unknown
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi
alipowasili eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero
wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare
kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya
uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi
baada ya kuwasili eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la
Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo
la Nteritare kwa upande wa Burundi kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa
programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.

Wengine ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna
Tibaijuka na Balozi wa Burundi nchini Tanzania Mhe Issa Ntambuka.
Rais
Pierre Nkurunzinza wa Burundi akisalimiana na Waziri wa Nishati na
Madini wa Tanzania Profesa Sospeter Muhongo eneo la mpaka kati ya
Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa
upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi
kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya
kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Wasanii
wa ngoma ya utamaduni kutoka Burundi wakiburudisha kwenye sherehe za
uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano
Agosti 27, 2014.
Rais
Pierre Nkurunzinza wa Burundi akisalimiana na baadhi ya Watanzania
walikuwepo eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero
wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare
kwa upande wa Burundi kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa programu ya
uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakipokea
nyimbo za Taifa za nchi zao eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la
Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo
la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa
programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Sehemu
ya umati wa wananchi wa Tanzania na Burundi kwenye sherehe za uzinduzi
wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27,
2014.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi wa Tanzania na Burundi katika
eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara
mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa
Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa
mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa meza kuu pamoja na Waziri wa Ardhi na
Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo na Naibu Katibu Mkuu Wizara Uchukuzi Dkt
Charles Tizeba eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero
wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare
kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya
uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi katika picha ya
kumbukumbu na wataalamu wa Tanzania na Burundi eneo la mpaka kati ya
Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa
upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi
kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya
kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakiangalia
moja ya alama katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la
Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo
la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa
programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi,
Profesa Anna Tibaijuka
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakitembelea
eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara
mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa
Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa
mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete
ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakiangalia
moja ya alama katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la
Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo
la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa
programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi,
Profesa Anna Tibaijuka
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakipata
maelezo na kuangalia vifaa vya upimaji eneo la mpaka kati ya Tanzania
na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa
Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe
za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano
Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na
Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakizindua
kwa pamoja eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero
wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare
kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya
uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi
wakipongezana kwa furaha katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na
Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa
Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe
za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano
Agosti 27, 2014. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi
wakichanganjya udongo na kujenga kwa pamoja alama katika eneo la mpaka
kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera
kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi
wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya
kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi na wananchi
wa nchi zao wakisimama wakati nyimbo za Taifa za Burundi na Tanzania
zikipigwa katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la
Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo
la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa
programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakijipatia
chakula cha mchana katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la
Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo
la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa
programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakiagana
katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani
Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa
upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya
uimarishaji wa mipaka ya kimataifa
2:21 AM
Unknown
Ethiopia na Kenya zimetangaza niya ya kutaka kuwa wenyeji wa kombe la
mataifa bingwa barani Afrika mwaka wa 2017 baada ya Libya kujiondoa.
Libya ilitangaza kauli hiyo baada ya mapigano kuchacha baina ya makundi mawili hasimu yaliyowanyima waandalizi fursa ya kujenga viwanja vipya vya mashindano hayo.
Ethiopia, ambayo imewahi kuwa mwenyeji wa mashindano hayo katika miaka ya 1962, 1968 na 1976, imesema kuwa itawasilisha rasmi ombi lake mara moja
Rasi wa Shirikisho la soka la Ethiopia Junedin Basha ameiambia BBCMichezo kuwa tayari taifa hilo linaviwanja viwili vyenye hadhi ya kimataifa (Addis Ababa na Bahir Dar), na hivyo hoja kuu itakuwa kukamilisha viwanja viwili vipya ambavyo tayari vinaendelea kujengwa.
"Serikali inaari ya kuyaleta mashindano hayo hapa Ethiopia ."alisema
Kenya kwa upande wake imetangaza niya ya kuandaa mashindano hayo kwa pamoja na Tanzania Uganda au Rwanda.
Shirikisho la soka barani Afrika limetangaza tarehe 30 Septemba kuwa siku ya mwisho ya mataifa kuwasilisha maombi yao.
Tangazo rasmi ya nani atakayeandaa mashindano hayo itakuwa mwakani

Subscribe to:
Posts (Atom)