Monday, September 28, 2015

Jumanne zipo Mechi 8 za Makundi E hadi H na Jumatano ni 8 za Makundi hadi A hadi D.
Mabingwa Watetezi Barca wako kwao Nou Camp kucheza na Bayer Leverkusen wakisaka ushindi wao wa kwanza baada ya kutoka Sare 1-1 na AS Roma katika Mechi yao ya kwanza ya kundi E Ugenini huko Italy.
Lakini Barca watatinga Mechi hii bila ya tegemezi wao mkubwa Lionel messi ambae ameumia Goti na anakisiwa kuwa nje kwa kipindi cha hadi Wiki 8.
Bayer Leverkusen walishinda Mechi yao ya kwanza kwa kuinyuka BATE Borislov 4-1.
Kwenye Kundi F, Arsenal, baada ya kuchapwa 2-1 Dinamo Zagreb wako kwao Emirates kucheza na Olympiacos ambayo ilianza kwa kuchapwa kwao 3-0 na Bayern Munich ambao wanacheza Nyumbani huko Munich na Dinamo Zagreb.
Chelsea, ambao walianza kwa kuinyuka Maccabi Tel Aviv 4-0 Uwanjani Stamford Bridge, wako Ugenini huko Ureno kucheza na FC Porto ambayo ndiyo Klabu iliyompa umaarufu Meneja wao wa sasa Jose Mourinho.
FC Porto walianza kwa Sare ya 2-2 Ugenini na Dynamo Kiev. 


UEFA CHAMPIONS LIGI
RATIBA
Jumanne 29 Septemba 2015

KUNDI E
Barcelona vs Bayer Leverkusen
BATE Borislov vs AS Roma

KUNDI F
Arsenal vs Olympiakos
Bayern Munich vs Dinamo Zagreb

KUNDI G
FC Porto vs Chelsea
Maccabi Tel Aviv vs Dynamo Kiev

KUNDI H

Lyon vs Valencia
Zenit St Petersburg vs KAA Gent

Jumatano 30 Septemba 2015
KUNDI A

Malmö FF v Real Madrid
Shakhtar Donetsk v Paris St Germaine

KUNDI B
CSKA v PSV
Man United vs VfL Wolfsburg

KUNDI C
1900 FC Astana v Galatasaray
Atletico Madrid vs Benfica

KUNDI D
Borussia Mönchengladbach vs Man City
Juventus vs Sevilla

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog