Monday, September 14, 2015


Real Madrid wameichakaza timu ya Espanyol bao 6-0, Bao tano zikifungwa na staa wake Cristiano Ronaldo.
Bao za Real zilifungwa na
Cristiano Ronaldo 7'
• Cristiano Ronaldo 17' Penati
• Cristiano Ronaldo dakika ya 20'
• Karim Benzema 28'
• Cristiano Ronaldo 61'
• Cristiano Ronaldo 81

Bao hizo zimemfanya awe ndio Mfungaji Bora katika Mechi za La Liga katika Historia ya Real Madrid kwa kumpiku Raul mwenye Bao 228 na sasa yeye ana Bao 230.
Leo Ronaldo alianza kwa kupiga Hetitriki ya ndani ya Dakika 13, ikiwa ni Hetitriki yake ya 29 kwenye La Liga akiendelea kushika Rekodi hiyo, kwa Bao za Dakika za 7, 17 na 20.
Karim Benzema ndie alieifungia Real Bao la 4 na Ronaldo kuongeza tena Bao 2 katika Dakika za 61 na 81.
Hii ni mara ya pili kwa Ronaldo kufunga Bao 5 katika Mechi baada ya Aprili 5 Mwaka huu pia kupiga 5 wakati Real ikiifunga Granada 9-1

Ligi kuu ya Uhispania imeendelea leo baada ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa kumalizika, Real Madrid walisafiri mpaka jijini Barcelona kwenda kucheza na Espanyol.
 
Mchezo uliopigwa katika dimba la Cornella El Plat umeshuhudia mwanasoka anayeshikilia taji la uchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo akifunga magoli 5 katika mchezo uliomalizika kwa Real Madrid kushinda 6-0.
 
Ilimchukua Cristiano Ronaldo dakika 20 tu kufunga hat trick katika dakika ya 7, 17 na 20, kabla ya Karim Benzema hajafinga goli la 4 katika dakika ya 28 na hivyo kupelekea Madrid kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa 4-0.
 
Kipindi cha Ronaldo akaongeza magoli mawili katika dakika ya 60 na 80 ya mchezo huo na hivyo kukamilisha ushindi wa 6-0
Timu zilipangwa hivi
Espanyol: Lopez, Arbilla, Alvaro, Ciani (Paco Montanes 46), Duarte, Victor (Joan Jordan 64), Javi Lopez (Canas 46), Alvarez, Salva, Gerard, Caicedo
Substitutes not used: Bardi, Juan Fuentes, Raillo, Sylla
Booked: Alvaro, Canas
Real Madrid: Navas, Carvajal, Pepe, Ramos (Varane 74), Marcelo, Casemiro, Modric (Kovacic 55), Isco, Bale, Ronaldo, Benzema (Vazquez 62)
Substitutes not used: Casilla, Kroos, Arbeloa, Jese
Scorers: Ronaldo 7, 17 pen, 20, 61, 80; Benzema 28

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog