Monday, September 14, 2015



Chelsea wakicheza huko Goodison Park Mjini Liverpool, Mabingwa Watetezi Chelsea Leo wametandikwa Bao 3-1 na Everton katika Mechi ya Ligi Kuu England na Bao zote za Everton zikifungwa na Steven Naismith alieingizwa Dakika ya 9 kumbadili Majeruhi Besic.
Mchezo ukikaribia kufika tamati Mashabiki wa Everton waliikebehi Chelsea na hasa Meneja wao Jose Mourinho kwa kuimba ‘Utafukuzwa kazi Asubuhi!’ na pia kuimba ‘Mnashuka Daraja!’
Everton walipata Bao la kwanza katika Dakika ya 17 mfungaji akiwa Steven Naismith aliegongeana vizuri na Galloway ambae alitia krosi Golini na Naismith kufunga kwa Kichwa.
Alikuwa tena Steven Naismith aliefunga Bao la pili katika Dakika ya 22 kufuatia pasi safi toka kwa Lukaku kwenda kwa Kone aliempa McCarthy aliemsogezea Naismith ambae aliachia kigongo cha chini toka Mita 25 na kumshinda Kipa Asmir Begovich.

Dakika ya 36 Chelsea walipata Bao kwa Shuti kali la Mita 40 la Nemanja Matic na kuifanya Gemu iende Haftaimu ikiwa 2-1.
Dakika ya 82, Naismith alipiga Bao lake la 3 kutokana na kusukiwa vizuri na ushirikiano wa Barkley, Stones na Lennon kutoka upande wa kulia.
Hadi mwisho Everton 3 Chelsea 1.
Huu ni mwanzo mbovu kabisa kwa Mabingwa Chelsea ambao katika Mechi 5 za Ligi wameshinda 1, Sare 1 na kufungwa 3.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog