Friday, September 25, 2015

Kabla ya dirisha la usajili halijafungwa mwezi August mwaka huu, barani Ulaya kulikuwa na stori tofauti tofauti kuhusiana na baadhi ya wachezaji nyota kuhusishwa kutaka kuvihama vilabu vyao na kujiunga na timu nyingine. Moja kati ya mastaa waliokuwa wanahusishwa kuhama timu zao ni Neymar ambaye alitajwa kuwa katika mipango ya Man United.
September 25 mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil anayekipiga katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania, amefunguka kuhusiana na mpango huo wa yeye kutaka kuhamia Man United katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August mwaka huu.
IwWEj
“Ni kweli tulikuwa na mazungumzo ya awali, lakini hakukuwa na nia ya dhati katika hili, awali nilisikia kuwa kulikuwa na ofa kwa ajili yangu lakini hakuna kilichofanyika kwangu”>>> Neymar
Afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Man United Ed Woodward alisafiri mapema mwezi August kwenda Barcelona kwa ajili ya kukamilisha usajili wa Pedro Rodriguez kabla ya nyota huyo kujiunga na Chelsea ila Ed Woodward inaripotiwa jumuisha mipango ya kumtaka Neymar.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog