Sunday, July 12, 2015


Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM umeteuwa majina matatu kati ya matano yaliyopendekezwa na wajumbe wa mkutano huo kwa ajili ya kuyajadili na hatimaye kupata jina moja la mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM.
Waliopendekezwa na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ni Dk. John Pombe Magufuli, Balozi Amina Salum Ali na Dk. Asha Rose Migiro ambao majina yao yatajadiliwa na Mkutano Mkuu ili kupata jina moja ambaye ndiye atakuwa mgombea wa Urais wa CCM.


Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowasa akimpongeza Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha Rose Migiro baada ya jina lake kupita katika mchujo wa tatu bora. (Picha zote na Joseph Senga)

Kutoka kushoto ni Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na Waziri Mkuu mstaafu, Samuel Malecela wakiwa katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM uliofanyika katika ukumbi wa White House mjini Dodoma.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akimfariji Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba ambaye hata jina lake halikuweza kuingia katika tano bora katika mchujo wa wagombea wa Urais wa CCM.

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowasa akibadilishana mawazo na Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe ndani ya ukumbi wa White House mjini Dodoma baada ya kumalizika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowasa ndani ya ukumbi wa Mkutano.

Wafuasi wa Lowasa wakiimba nje ya Ukumbi wa Mkutano.
Polisi wakiimarisha ulinzi.

Rais Jakaya Kikwete akiwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

January Makamba akiwashukuru wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM baada ya kumalizika kwa mkutano huo ambao uliengua jina lake.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog