Sunday, July 12, 2015


KLABU ya Real Madrid imetangaza kwamba kipa gwiji, Iker Casillas amekubali kuhamia FC Porto ya Ureno.
Vigogo hao wa Hispania wametangaza hilo kupitia tovuti yao jana kwamba kipa huyo mwenye umri wa miaka 34 ataondoka sambamba na kumshukuru kwa mchango wake.
“Tumekubali uhamisho wa klabu ya Ureno kwa Iker Casillas,” imesema Real. 
Real Madrid imeposti picha kwenye akaunti yake ya Twitter kumshukuru Casillas kwa mchango wake katika klabu hiyo ikiwa ni pamoja na kuiwezesha timu kushinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, matano ya La Liga na matatu ya Copa del Rey.

Kuondoka kwa Casillas kwenda timu ya Ureno, Porto kunaweza kuongeza kasi ya Real kufukuzia saini ya kipa wa Manchester United, David de Gea.
“Kwa Real Madrid leo ni siku, kabla na juu ya yote, kwa kweli huyu hatakuwa mmoja wa makipa bora katika klabu yetu, bali ni kipa bora katika historia ya Real Madrid na soka ya Hispania,”.
Casillas anaondoka Bernabeu baada ya miaka 16 akiidakia timu hiyo mechi 725 kwenye mashindano yote.
Wakati huo huo: Real Madrid imemtambulisha beki wa pembeni Mbrazil, Danilo kutoka Porto iliyemsajili kwa ada ya Pauni Milioni 22.6, akisaini Mkataba wa miaka sita.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog