Klabu ya Arsenal ya Uingereza miaka kadhaa nyuma ilikuwa ni nadra sana kukuta inasajili mchezaji kwa gharama za juu ila kufuatia falsafa za kocha Arsene Wenger
ambae anaaminika kuwa hakutaka kukubali kuwa soka limebadilika na
wachezaji wananunuliwa kwa gharama za juu, yeye alikuwa akiendelea
kuwatumia wachezaji makinda na kununua wachezaji kwa gharama nafuu.
Wenger alionekana kuanza kukubali kwamba soka limebadilika baada ya kuwasajili Mesut Ozil kutokea Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 42 mwaka 2013 na kumsajili Alexis Sanchez kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 35 akitokea FC Barcelona.
Kufuatia mpango wa kuboresha kikosi hicho cha Emirates mkurugenzi wa Arsenal Lord Harris amethibitisha kuwa Arsene Wenger ana uwezo wa kumsajili mchezaji yoyote duniani kwa sasa.
Licha ya Wenger kukubali kuwa Arsenal kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ikishindwa kutwaa taji la Ligi Kuu Uingereza ila Lord Harris amethibitisha Arsenal kuwa imetenga bajeti ya pound milioni 200 kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao.
“Arsene Wenger
anaweza kumnunua mchezaji yoyote duniani, suala la fedha lilikuwa gumu
kwetu wakati tunahamia Emirates lakini sasa tuko huru… katika account ya
benki tuna pound milioni 200. Hakuna mpango wa kumsajili mchezaji
yoyote isipokuwa kama atapata mchezaji nyota kama Ozil au Sanchez,
lakini anaangalia mmoja kati ya wachezaji ambao
hawapatikani”>>> Lord Harris
0 maoni:
Post a Comment