Saturday, May 9, 2015


Tayari Ligi Kuu Vodacom inae Bingwa, Yanga, Mshindi wa Pili, Azam FC, na Mshindi wa Tatu, Simba, lakini kazi kubwa ipo leo hii Jumamosi kwenye Mechi za mwisho kabisa za Msimu kuamua Timu ipi moja itaungana na Polisi Moro kuteremka Daraja.
Yanga walishatwaa Ubingwa tangu Wiki iliyopita na Msimu ujao watawakilisha kwenye CAF CHAMPIONS LIGI na Azam FC, ambao wamepoteza Taji lao, wameshika Nafasi ya Pili na hivyo watacheza Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.
Kwa Msimu huu Timu mbili zitashushwa Daraja na Timu 4 kupandishwa ili kufanya idadi ya Timu za Ligi Kuu Vodacom kuwa 16 Msimu ujao badala ya 14 za sasa.
Timu 4 zilizofuzu kupanda Daraja na kucheza Ligi Kuu Vodacom Msimu ujao ni Majimaji ya Songea, Mwadui ya Shinyanga, African Sports ya Tanga na Toto Africans ya Mwanza.
Timu moja ambayo itaungana na Polisi Moro kuporomoka Daraja kutoka Ligi Kuu Vodacom ni moja kati ya Timu 5 ambazo ni Ruvu Shooting, Prisons, Stand United, Ndanda FC na Mgambo JKT.
Ligi Kuu Vodacom itamalizika Jumamosi hii Mei 9, 2015
LIGI KUU VODACOM
RATIBA
Jumamosi Mei 9
Ratiba hiyo!Mwali wa Yanga SC

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog