Saturday, May 9, 2015


LIGI KUU ENGLAND Wikiendi hii inaanza safari yake ya kumalizia Raundi zake 3 za mwisho wakati Bingwa, Chelsea, anatarajiwa kukabidhiwa Kombe lao Jumapili Uwanjani kwao Stamford Bridge wakicheza na Liverpool ambayo bado ina matumaini ya kufuzu 4 Bora.
Jumamosi zipo Mechi 7 ambazo nyingine ni muhimu kwa Timu zinazotaka kujinusuru kutoshushwa Daraja na hizo, kimahesabu, ni Timu 9 ambazo zipo kwenye hatari hiyo.Timu hizo ni kuanzia Crystal Palace, iliyo Nafasi ya 12, zikifuatia West Bromwich Albion, Aston Villa, Newcastle, Leicester City, Hull City na zile 3 za mkiani, Sunderland, QPR na Burnley.
Huko juu, baada ya Chelsea kutwaa Ubingwa na kujihakikishia kuwa moja ya Timu 4 zitakazocheza Ulaya kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao, vita imebaki kupatika 3 zipi nyingine zitaungana nao.
Ingawa Man City na Arsenal wana nafasi nzuri sana kuwemo 4 Bora, kimahesabu lolote linaweza kutokea na hivyo wanahitaji ushindi ili kujihakikishia kuwemo.
Kazi kubwa ipo kwa Man United, walio Nafasi ya 4, wakiwa Pointi 4 mbele ya Timu ya 5 Liverpool na ambao pia, kimahesabu wanaweza kupitwa na hata Tottenham, walio Nafasi ya 6 na Southampton, walio Nafasi ya 7.
Jumamosi, Man United wako Ugenini huko Selhurts Park kuivaa Crystal Palace wakitafuta ushindi wao wa kwanza baada kudundwa Mechi 3 mfululizo.
Ikiwa Man United watashinda Mechi hiyo na Liverpool kutetereka huko Stamford Bridge wakicheza na Mabingwa Chelsea, basi uhakika wa Man United kucheza UEFA CHAMPIONS utakuwa wa matumaini ya kutosha.

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
Jumamosi Mei 9

14:45 Everton vs Sunderland
17:00 Aston Villa vs West Ham
17:00 Hull vs Burnley
17:00 Leicester vs Southampton
17:00 Newcastle vs West Brom
17:00 Stoke vs Tottenham
19:30 Crystal Palace vs Man United

Jumapili Mei 10
15:30 Man City vs QPR
18:00 Chelsea vs Liverpool
Jumatatu Mei 11
22:00 Arsenal vs Swansea

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog