Friday, April 17, 2015


www.bukobasports.comFA CUP
Nusu Fainali
Mechi zote kuchezwa Wembley, London

Jumamosi Aprili 18
19:20 Reading v Arsenal
Jumapili Aprili 19
18:00 Aston Villa v Liverpool
Michezo yote ya FA CUP wikiendi hii kuchezewa kwenye Uwanja wa Wembley, London
Huko Uingereza, Mechi ya Nussu Fainali ya FA CUP ya Reading vs Arsenal itaonyeshwa na TV ya BBC1 na ile ya Ligi ya Chelsea vs Man United itarushwa na Sky Sports.
Kutokutenganishwa kwa muda wa kuanza Mechi hizi kumezua mjadala mkubwa huko England na Wadau mbalimbali kuponda uroho wa Makampuni ya TV katika ushindani wao.
Akiongelea kuhusu mgongano huo, Arsene Wenger, Meneja wa Arsenal, ameponda uamuzi wa kuzigonganisha Nusu Fainali ya FA CUP na Mechi kubwa ya Ligi.
Amesema: "Lazima wangefanya uamuzi. Hili halipaswi kutokea katika Nchi moja. Kombe kubwa la FA CUP linagonganishwa na Mechi kubwa ya Ligi!"

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog